14 Novemba 2023 - 18:57
Siku 37 za vita vya Gaza

Jumapili vita vya Ghaza viliingia katika siku ya 37 , huku utawala wa Kizayuni ukiendeleza mashambulizi na jinai zake za kinyama dhidi ya wakazi wa Gaza na hasa kwa kushambulia kikatili hospitali, shule, kambi za wakimbizi, wahudumu wa afya, wagonjwa na majeruhi kwa uungaji mkono wa moja kwa moja wa Marekani.

Wanajeshi katili wa Kizayuni wanaendelea kuzingira hospitali za Ghaza, ikiwemo hospital ya al-Shifa, na wanampiga risasi mtu yeyote anayejaribu kuondoka au kuingia katika majengo ya hospitali hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Ukanda wa Ghaza ameeleza kuwa, hospitali ya al-Shifa imekabiliwa na mashambulizi makali zaidi ya anga ya utawala wa Kizayuni, na wanajeshi vamizi wako umbali wa mita 100 kutoka hospitali hiyo ambapo wanamlenga mtu yeyote ambaye anaingia au kutoka hospitalini hapo.

Hospitali nyingine za Gaza zina hali kama hiyohiyo ya Hospitali ya al-Shifa, na Hilali Nyekundu ya Palestina imeripoti kwamba vifaru vya Israel viko umbali wa mita 20 kutoka hospitali ya Al-Quds ambapo wanajeshi wa utawala ghasibu wanawafyatulia risasi za moja kwa moja wakimbizi waliokimbilia usalama wao katika jengo hilo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) pia limeonya kwamba maisha ya watoto milioni 1 wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza yako hatarini kutokana na kukaribia kusambaratika kabisa sekta za huduma na afya za eneo hilo.

Huku ikiashiria kuzima mashine za dharura katika hospitali za Al-Nasr na Al-Rentisi ambazo ni maalumu kwa  watoto, UNICEF imetangaza kuwa kuendelea kushambuliwa hospitali hizo kunatishia maisha ya watoto hasa walio na matatizo ya figo (wanaofanyiwa dialysis) na wanahitajia uangalizi maalum. Aidha, maelfu ya watoto kaskazini mwa Gaza wanakabiliwa na hali mbaya sana kutokana na kukosa mahali salama pa kwenda, kuishi chini ya mashambulizi makali na kukosena huduma za kimsingi za maisha.

342/